Saturday, July 12, 2014

BIN SLUM AHAMIA AFRICAN SPORTS, COASTAL UNION CHAZIDI KUNUKA

MGOGORO wa Coastal Union umechukua hatua mpya baada ya kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Mohamed Bin Slum kuhamia kwa mahasimu, African Sports, pia ya Tanga.

Inafahamika familia ya Bin Slum ni Coastal damu, lakini baada ya mgogoro uliobuka baina ya familia hiyo na uongozi wa sasa wa klabu hiyo chini ya Mwenyekiti, Hemed Hilal ‘Aurora’- mpasuko umeibuka.
Bin Slum wamekuwa wakiisaidia Coastal kwa hali na mali chini ya uongozi wa Aurora, ikiwemo kusajili wachezaji na mambo mengine, lakini mwishoni mwa msimu, yakaibuka makubwa.
Kadi ya uanachama ya Mohammed Bin Slum mbele na nyuma


Thursday, July 10, 2014

Kurasa za mwanzo na mwisho magazetini leo July 10 2014

.
.
Kama kawaida ndangale.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.

USAJILI LIGI KUU YA ENGLAND FULL




BPL_LOGO
KLABU za Ligi Kuu England zipo kwenye heka heka kubwa za kusajili Wachezaji wapya kwa ajili ya Msimu mpya wa 2014/15 unaoanza Agosti 16 lakini Dirisha la Uhamisho litafungwa rasmi Septemba 1 Saa 7 Usiku Saa za Bongo.

PATA WACHEZAJI WALIOHAMA/KUHAMIA KWA KILA KWA KLABU ZOTE 20:
+++++++++++++++++++++++++++++++
ARSENAL
NDANI
NJE
Lukasz Fabianski
(Swansea City) BURE
Bacary Sagna
(Manchester City) BURE

Kilichojiri kwenye mechi ya Uholanzi vs Argentina

20140710-015925-7165023.jpg
Baada ya jana kushuhudia kalamu ya magoli kwenye mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia kati ya Brazil na Ujerumani, leo hii imepigwa nisu fainali ya pili kati ya Argentina na Uholanzi.

Matokeo ya mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Sao Paolo ni ushindi uliotokana na mikwaju ya penati wa 4-2 kwa Argentina.

Mechi hiyo ilikuwa ya kukamiana na kucheza kwa kujihami kwa timu zote mbili iliisha kwa sare tasa katika dakika 120 na hivyo ikaamuriwa ipigwe mikwaju ya penati.

Waliopata penati kwa Argentina ni Messi, Aguero, Garay, na Rodriguez wakati Robben na Dirk Kuyt wakifunga penati mbili za uholanzi huku Vlaar na Sneijder wakikosa.

Argentina sasa itaenda kucheza na Ujerumani fainali jumapili hii, wakati Uholanzi wakikutana na Brazil jumamosi kugombea medalinya mshindi wa 3.

Sunday, July 6, 2014

KIONGOZI WA CHADEMA KANDA YA MAGHARIBI ASHAMBULIWA

Makamu Mwenyekiti Uenezi CHADEMA, Kanda ya Magharibi, Deogratius Liyunga akiwa amelazwa katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana (Picha na Editha Karlo).
Na Editha Karlo, Kigoma
WATU wasiojulikana wamemvamia na kumpiga pamoja na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia vitu vyenye ncha kali Makamu Mwenyekiti wa uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Magaharibi, Deogratius Liyunga na kupelekea kulazwa katika Hospita ya Mkoa wa Kigoma (Maweni).

Tukio hilo limetokea jana majira ya  saa tano usiku katika eneo la Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji,wakati kiongozi huyo akiwa njiani kurudi nyumbani

UMOJA WA WANAWAKE LUDEWA{UWALU} WATOA MISAADA KATIKA HOSPITALI YA LUDEWA



mganga mkuu wa wilaya Bwana Msengi katikati akipoke misaada hiyo