
mganga mkuu wa wilaya Bwana Msengi katikati akipoke misaada hiyo
![]() |
UWALU wakionesha baadhi ya vifaa hivyo |
![]() |
Bwana msengi akizungumza jambo na wanawake wa UWALU |
Umoja
wa wanawake ludewa [UWALU] waishio dare es salaam Umetoa misaada
mbali mbali ya vifaaa katika hospitali ya wilayani hapa ukilenga
zaidi huduma ya akina mama na watoto.
amesema
hayo hii leo katibu wa chama hicho B, Sarah wakati akisoma risala
fupi mbele ya mganga mkuu wa wilaya Bw.Msengi Mwendo ambapo amesema
chama hicho kilianzishwa na akina mama hao kwa lengo la kushiriki
katika shughuli za kijamii,kama vile kuchangia
katika
huduma za afya,elimu pamoja na maafa.
Akikabidhi
vifaa mbele ya mganga mkuu wa wilaya ludewa B, Sarah amesema kuwa
umoja huo umetoa vifaa kama vifaa
kama vile Vitanda vya kuzalishia,vitanda vya kujifungulia,mashuka90,
blanketi 50 pamoja na troli ya kubebea dawa.
Aidha
kwa upande wa mganga mkuu wa hospitali hoyo Bw.Msengi ameushukuru
umoja wa aikina mama hao kwani wamegusa nyanja ambazo mara nyingi
kumekuwa na na changamoto nyingi katika utoaji huduma hususani kwa
aikana mama wajawazito pamoja na watoto wadogo ukizingatia ludewa
sasa imekuwa na ongezeko kubwa la watu kutoka sehemu mbalimbali.
Pia
bw, Msengi Ameiomba jamii kwa ujumla kuanzisha vikundi mbali mbali
kwani vimekuwa ni msaada mkubwa katika kuchangia na kuchochea huduma
bora za kijamii.
No comments:
Post a Comment