Na Editha Karlo, Kigoma
WATU wasiojulikana wamemvamia na kumpiga pamoja na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia vitu vyenye ncha kali Makamu Mwenyekiti wa uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Magaharibi, Deogratius Liyunga na kupelekea kulazwa katika Hospita ya Mkoa wa Kigoma (Maweni).

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa
tano usiku katika eneo la Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji,wakati kiongozi
huyo akiwa njiani kurudi nyumbani
kwake akitokea eneo la Mwanga
kuangalia mechi za kombe la Dunia.
Akiongea na mtandao huu wodini na
alipolazwa juu ya tukio hilo,kiongozi huyo alisema kuwa alibakiza hatua
25 iliaweze kuingia nyumbani kwake ghafla walitokea watu wanne,mmoja
alimvamia na kumkaba shingo huku wale wengine wakimshambulia kwa
kisu,nyembe na ubao.
Alisema mbali ya watu hao kumpiga na
kumjeruhi lakini walimpora fedha kiasi cha shilingi 63,000 ingawa
hawakufanikiwa kumpora simu yake ya mkononi iliyokuwa mfukoni.
Baada ya watu hao waliomvamia kuondoka
alifanya mawasiliano kwa watu wake wa karibu wakiwemo wanachama wa
CHADEMA ambao walifika eneo la tukio na kumkimbiza Hospital kwaajili ya
matibabu.
Makamu Mwenyekiti alisema kuwa tukio hilo
lililomkuta linahusiano mkubwa na masuala ya kisiasa kwani kabla ya
tukio hilo amekuwa akipokea ujumbe mfupi wa maneno ya vitisho kwenye
simu yake ya mkononi kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa ni wananchama wa
chama kipya cha ACT.
''Mimi hiyo taarifa sijaipata ofisini kwangu bado ndo nina isikia kutoka kwako ngoja nifuatilie
No comments:
Post a Comment